Wednesday, December 12, 2012

YOTE HAYA NI MATUNDA YA CCM


RAIS KIKWETE APOKEA MAJENGO MAPYA MATATU YA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO DAR ES SALAAM

Tuesday, December 11, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo Mhe John Mnyika na Balozi wa Korea kwa pamoja wakifungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Balozi wa Korea kwa pamoja wakitembelea sehemu ya chumba cha upasuaji mkubwa chenye vifaa vya kisasa baada ya kufungua  rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Ilala ijini Dar es salaam leo December 12, 2012


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete wakimsalimia mzazi aliyejfungua salama alipofanya ziara baada ya kufungua  rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipewa saluti alipowasili kufungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Balozi wa Korea kwa pamoja katika picha ya pamoja na madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Mnazi mmoja  baada ya kufungua  rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Ilala ijini Dar es salaam leo December 12, 2012

KINANA NA SEKRETARIETI YAKE WAKUTANA NA MAKATIBU WA CCM WA MIKOA‏

Monday, December 10, 2012
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai akisalimiana na Katibu wa NEC, Siasa na Mambo ya Nje, Asha-Rose Migiro, kabla ya kuanza kikao cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Muhammed Seif Khatib. (Picha na Bashir Nkoromo).

Makatibu wa CCM wa mikoa wakiwa kwenye mkutano wao na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao chake cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo, Desemba 11, 2012, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na wengine kutoka kushoto ni Makatibu wa NEC,  Asha-Rose Migoro (Siasa na Mambo ya Nje), Zakia Meghji (Uchumi na Fedha), Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai. (Picha na Bashir Nkoromo)

MATUKIO MBALI MBALI YA SHEREHE ZA MIAKA 51 YA UHURU

Sunday, December 9, 2012
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere kwenye maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru.

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakipiga Gwaride kwa mwendo wa haraka.

Gozibety Mbwele (3)akipiga ngoma kwa umakini na kuwa kivutio cha hali ya juu,mbele yake ni Nyamburi Mganga (5) akicheza kwa umaridadi, watoto hawa ni wasanii kutoka kundi la Utandawazi,Mwanza

Kikundi cha ngoma kutoka Rwanda kikitoa burudani ya kipekee uwanjani hapo.

Watoto hodari wakishiriki katika halaiki kwenye sherehe ya kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha wageni waalikwa kutoka mataifa rafiki waliofika kushuhudia sherehe za miaka 51 ya Uhuru.

No comments:

Post a Comment