MWENYEKITI WA CCM, NDUGU JAKAYA KIKWETE AKABIDHI KADI 1138 KWA WANACHAMA WAPYA, LINDI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi akihutubia katika moja ya Mikutano yake ya hadhara katika Ziara yake Mkoani Lindi. |
Na. Mwandishi wetu, Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewapokea na kuwakabidhi kadi wanachama wapya 1138 walipojiunga na Chama Cha Mapinduzi, katika wilaya za Liwale na Nachingwea Mkoani Lindi.
Mwenyekiti Huyo wa Chama Tawala aliwapokea wanachama hao wapya baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wake wa hadhara katika uzinduzi wa Boma la Wananchi Nachingwea na mkutano wa Hadhara Liwale, ambapo wanachama hao wapya walikabidhiwa kadi za chama na kisha kuapishwa kwa Imani na Ahadi za Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Rais yupo katika Ziara ya Kikazi Mkoani humo ambapo alishiriki maazimisho ya siku ya Ukimwi Duniani tarehe 01st Dec 2012 kisha kufanya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo ya wananchi Mkoani Lindi pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali na Changamoto zinazoikabili Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Rais anaendelea na Ziara yake Mkoani umo ambapo leo yupo katika wilaya ya Kilwa ambayo iko chini ya Mheshimiwa Abdallah Ulega aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani. Mheshimiwa Rais anategemea kumalizia ziara yake wilayani Kilwa,alasiri ya leo, tarehe 5th Dec 2012
No comments:
Post a Comment