Tuesday, December 18, 2012

KATIBU WA NEC ZAKIA HAMDANI MEGHJI AKAGUA RASLIMALI ARDHI YA CCM ZANZIBAR


MJUMBE wa Kamati Kuu ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa wa Uchumi na Fedha ndugu Zakia Hamdan Meghji, jana alifanya ziara Kisiwani Unguja kwa lengo la kuangalia raslimali ardhi ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.

Akiwa amefuatana na Katibu wa amati Maalum ya NEC wa Idara ya Uchumi na Fedha Ndugu Seif Suleiman Mohamed, mama Meghji alitembelea maeneo mbali mbali ya ardhi ambayo yametengwa mahusus kwa ajili ya kitegauchumi wa chama hicho na hivyo kujinasua katika suala zima la utegemezi.

Katika ziara hiyo, Katibu huyo wa NEC alitemelea viwanja vilivyopo mbele ya Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Nyumba ya kumbukumbu ya Shirazi Association iliyopo Kijangwani, viwanja vya Mbweni, Tunguu na kumalizia kwa kutembelea mradi wa Chama huko Maisara.

Mama Meghji ameelezea kufarajika kwake kutokana na viwanja hivyo na kuahidi kuwa atafanya kila linalowezekana kuhakikisha maeneo hayo yanajengwa majengo ya kisasa kabisa yatakayotumika kama kitegauchuni wa Chama hicho.

Mapema Mkuu wa Utawala wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Salum Khatib Reja, alimweleza Katibu huyo wa NEC kwamba iwapo CCM itayatumia vizuri maeneo hayo, ni dhahiri Chama kitakuwa na uwezo mkubwa kifedha hapo baadae.



AFISI KUU YA
CCM ZANZIBAR
by Ali Ndota
S.L.P.875,
ccmchama@gmail.com


No comments:

Post a Comment