RAIS AZINDUA DAHARIA ZA SHULE YA WASICHANA YA NACHINGWEA.
Wednesday, December 5, 2012
Kutoka LINDI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndugu Jakaya M. Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Lindi ambapo amehudhuria Maazimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, ambapo kitaifa yamefanyika Mkoani hapa na pia anakagua na kufuatilia mipango na miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Miongoni mwa Miradi aliyozindua ni pamoja na Daharia ya Shule ya Wanawake Nachingwea iliyopo eneo la Bomani wilayani Nachingwea. Shule hiyo maaalum ya Wanawake imejengwa kwa nguvu za Wananchi wa Nachingwea wenyewe kwa kuchangishana kwa kushirikiana na Serikali.
Ujenzi wa Shule hiyo ulianza 2010 kutoka katika ruzuku ya Serikali katika mpango wa Serikali kuwainua na kuwawezesha wanawake kwa kuwapa fursa za Elimu kwa kuangalia namna ya kukabiliana na Changamoto zinazowakabili watoto wa kike, kama mimba za utotoni,umbali na mkakati wa kuongeza idadi ya watoto wa kike mashuleni.
Mheshimiwa Rais alitoa msaada wa pesa taslimu na ahadi ya kujenga Maabara, Viwanja vya michezo, Uzio, Jengo la Utawala, Bweni na Kuongeza Idadi ya Walimu. Pia aliipongeza Halmashauri ya wilaya hiyo kwa kupata wazo la kuendeleza majengo yaliyoachwa magofu kwa kutengeneza Shule hiyo.
Baada ya Uzinduzi huo Mheshimiwa aliendelea na ratiba yake ya kuhudhuria na kufanya Uzinduzi wa Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika maeneo mengine ya Mkoa wa Lindi.
No comments:
Post a Comment