Wednesday, December 19, 2012

TAARIFA RASMI … CCM


                                                           
                                                            TAARIFA RASMI … CCM                           15/12/2012
                                               
KAMATI Maalum ya NEC ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, leo imefanya kikao kilichokuwa chini ya Uenyekiti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Taarifa iliyotolewa na Afisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai, imesema kikao hicho cha kawaida cha siku moja,  pamoja na mambo mengine, kilipokea na kujadili kwa kina taarifa mbalimbali kutoka Idara na Vitengo vya Chama hicho.

Kikao pia kimefanya Mabadiliko katika Safu yake ya Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Zanzibar. Wajumbe walioteuliwa kuunda Sekretarieti hiyo mpya ni hawa wafuatao :-

1.       Ndugu Haji Mkema Haji - Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya           Organaizesheni.
2.       Ndugu Waride Bakari Jabu - Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara          ya Itikadi na Uenezi
3.       Ndugu Hamad Masauni Yussuf - Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa    Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) na
4.       Ndugu Seif Shaaban Muhamed - Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa   Idara ya Uchumi na Fedha.

Aidha, Kamati Maalum ya NEC kwa kauli moja imempongeza kwa dhati kabisa Rais wa Zanzibar (Awamu ya Saba) Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kufuatia kuchaguliwa kwake na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, uliofanyika Mjini Dodoma Novemba 11 - 13, 2012, kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar baada ya kupata kura zote za ndio.

Sambamba na hilo, kikao pia kimewapongeza Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu huo, kwa kumchagua kwa mara nyengine tena Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mwenyekiti wa CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo (2012 - 2017).   

Kikao kimempongeza kwa dhati kabisa Makamu Mwenyekiti (Mst.) wa CCM Zanzibar kwa kazi nzuri  ya kuwaongoza Wana CCM kwa kipindi chote cha miaka kumi (10) iliyopita tena kwa mafanikio makubwa.  Aidha, kikao kimemtakia kila la kheri yeye na familia yake na kumuomba Mwenyezi Mungu amjaalie salama na amani muda wote wa maisha yake.

Aidha, Chama Cha Mapinduzi kimempongeza kwa dhati kabisa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Ali Muhamed Shein kusimamia na kuimarisha masuala  ya Amani na Utulivu, Utekelezaji wa Ilani pamoja na kuisimamia ipasavyo Serikali yake na kuzishughulikia kero mbali mbali zinazowagusa wananchi yakiwemo matatizo ya ardhi.

Mwisho.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


……………….
(Vuai  Ali  Vuai),
Naibu Katibu Mkuu - CCM,
ZANZIBAR.

a good president of Tanzania Jakaya Kikwete in White House

WORLD BANK PRESS RELEASE WIND EAST AFRICA SINGIDA WIND PROJECT


The president of the United Republic of Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete congratulates the Wind East Africa team on the progress made with the Singida 100MW Wind Project after receiving an update on November 4th 2011 at the Singida State House. Left to Right. Said Abdallah (Project Director), Simon Magesa [Project Coordinator-Singida] Rashid Shamte (Founder -Project Director), Mark Gammons (Project Director), Jayce Kaiser (Project coordinator) (Photo:/ State House)
 
 
by Iddi Thabit Amour
Zanzibar
 

Tuesday, December 18, 2012

KATIBU WA NEC ZAKIA HAMDANI MEGHJI AKAGUA RASLIMALI ARDHI YA CCM ZANZIBAR


MJUMBE wa Kamati Kuu ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa wa Uchumi na Fedha ndugu Zakia Hamdan Meghji, jana alifanya ziara Kisiwani Unguja kwa lengo la kuangalia raslimali ardhi ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.

Akiwa amefuatana na Katibu wa amati Maalum ya NEC wa Idara ya Uchumi na Fedha Ndugu Seif Suleiman Mohamed, mama Meghji alitembelea maeneo mbali mbali ya ardhi ambayo yametengwa mahusus kwa ajili ya kitegauchumi wa chama hicho na hivyo kujinasua katika suala zima la utegemezi.

Katika ziara hiyo, Katibu huyo wa NEC alitemelea viwanja vilivyopo mbele ya Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Nyumba ya kumbukumbu ya Shirazi Association iliyopo Kijangwani, viwanja vya Mbweni, Tunguu na kumalizia kwa kutembelea mradi wa Chama huko Maisara.

Mama Meghji ameelezea kufarajika kwake kutokana na viwanja hivyo na kuahidi kuwa atafanya kila linalowezekana kuhakikisha maeneo hayo yanajengwa majengo ya kisasa kabisa yatakayotumika kama kitegauchuni wa Chama hicho.

Mapema Mkuu wa Utawala wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Salum Khatib Reja, alimweleza Katibu huyo wa NEC kwamba iwapo CCM itayatumia vizuri maeneo hayo, ni dhahiri Chama kitakuwa na uwezo mkubwa kifedha hapo baadae.



AFISI KUU YA
CCM ZANZIBAR
by Ali Ndota
S.L.P.875,
ccmchama@gmail.com


Friday, December 14, 2012

ZIARA YA SADIFA YAMALIZIKA PEMBA JANA

Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa na uwongozi wake aliofuatana nao akiwemo mh. Shaka H.Shaka M.kiti uvccm mkoa magharibi na diwani wa fuoni. ulikua pemba zaidi kuhusu safari hii nitakujuvya. pemba oyeeeeeee. sadifa oyeeeeeeee

HUYU NDIE SADIFA

KHAMIS SADIFA JUMA  MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA.

 

Dk. Sheni akimpongeza Khamis Sadifa Juma, baada ya kutangazwa Mshindi wa kuwa Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa, katika uchaguzi uliofanyika jana mjini Dodoma. (Picha na Bashir Nkoromo).
Mjumbe wa Kamati Kuu, Rais wa Zanzibar, Dk. Shein akiwa na Mwenyekiti mpya wa UVCCM,  Khamis Sadifa Juma na Makamu Mkt UVCCM, Mboni Mhita baada ya viongozi hao wapya wa Umoja huo kutangazwa kuwa washindi leo katika uchaguzi mkuu wa UVCCM uliofanyika jana mjini Dodoma. 
 Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti UVCCM Beno Malisa akimpongeza Khamis Sadifa Juma, baada ya kutangazwa Mshindi wa kuwa Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa, katika uchaguzi uliofanyika jana mjini Dodoma.
Kamanda wa Chipukizi Kingunge Ngombale-Mwiru akijadili jambo na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama wakati wa kutangazwa matokeo.
Katibu Mkuu wa UVCCM Martine shigela akimkaribisha meza kuu Khamis Sadifa Juma bada ya kutangazwa mshindi.

MPANGO MZIMA UVCCM JINSI DODOMA ILIVYOKUA

NAPE ALINOGESHA MKUTANO MKUU WA UVCCM DODOMA.


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi maalum Mwakilishi kutoka chama tawala cha  Zimbabwe Chipanga Kudzanai, kutambua mchango wa chama hicho kwa CCM, wakati wa Mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo  Okt 23, mjini Dodoma.
Mjumbe kutoka mkoa wa Mwanza, akipiga kura kuchagua Mwenyekiti, wakati wa Mkutano Mkuu wa UVCCM mjini Dodoma.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akicharaza gita zito la besi na bendi ya Vijana Jazz wakati wa Mkutano Mkuu wa nane wa UVCCM kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela akitoa utaratibu kabla ya kuanza uchaguzi mkuu wa jumuia hiyo leo mjini Dodoma.
Shamrashamra za Vijana kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere katika mkutano wa nane wa UVCCM mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM mjini Dodoma leo.
Wagombea waliokuwa wanawania nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM. Kutoka kushoto, Lulu Abdallah Mshamu ambaye alijitoa wakati akijieleza kwa wajumbe,Khamis Sadifa Juma na Msaraka Rashid Simai ambao ndio waliochuana.
-Wajumbe ukumbini wamwita ‘jembe’
- Anogesha mkutano kwa kucharaza gita na Vijana Jazz 
NA MWANDISHI WETU
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, amenogesha Mkutano mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM, UVCCM unaoendea mjini  Dodoma.
Licha ya viongozi wengi kushangiliwa wakati wa kuingia ukumbini, nderemo na shamaramshamra zililipuka zaidi kutoka kwa wajumbe wa Mkutano huo wakati Nape alipotangazwa kuwasili.
“Jembe, jembe, jembe”, wajumbe walisikika wakilipuka na kumshangilia baada ya Mkuu wa Umahasishaji na Chipukizi wa UVCCM, Esther Bulaya alipotangaza kuwasili kwa Nape ukumbini.
Ukumbi ulilipuka zaidi Nape alipopanda jukwaani na kuliungurumisha gita zito la besi, wakati Bendi ya Vijana Jazz ilipokuwa ikitumbuiza wimbo maalum, baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwasili ukumbini.
Viongozi wengine walioonyesha kuwakuna wajumbe wa mkutano huo wa vijana ambao ni wa Uchaguzi Mkuu ni pamoja, na Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma.
Baada ya mkutano kufunguliwa na Rais Kikwete, uchaguzi uliendelea ambapo leo, wanatarajiwa kupatika viongozi wapya wa UVCCM ngazi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Ujumbe wa Baraza Kuu UVCCM na wawakilishi kwenye jumuia zingine.
Katika nafasi ya Uwenyekiti ushindani ulihamia kwa wagombea wawili Msaraka Rashid Simai, Khamis Sadifa Juma baada ya mgombea mwingine Abdallah Lulu Mshamu kujitoa wakati wa kujieleza kwa wajumbe ukumbini.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wamechuana Ally Salum Hapi, Paul Christian Makonda Mboni Mohamed Mhita wakati nafasi zingine ni, Halmashauri Kuu ya Taifa Viti sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea 22, Nafasi ya Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39 na viti vitano Zanzibar wagombea 14,  Uwakilishi Wazazi Taifa na Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.